Michezo

CAF yaitetea RS Berkane

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipa ushindi wa mabao 3-0 timu ya RS Berkane ya Morocco dhidi ya USMA Alger ya Algeria, baada ya mchezo kati yao wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopaswa kuchezwa Aprili 21, 2024 kushindikana kutokana na sababu za kisiasa.

RS Berkane

Mamlaka za soka Algeria na serikali zilizuia jezi za Berkane zenye ramani ya Morocco wakisisitiza kuwa hawaitambui ramani ya Morocco iliyopo kwenye jezi za Berkane kwa sababu inajumuisha eneo la Sahara Magharibi na wanaamini kwamba Morocco kudhibiti eneo hilo ni haram.

USM Alger

CAF wameitaka USMA Alger kusafiri kuelekea Morocco kucheza mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa Aprili 28, 2024 na endapo hawatafika kwenye mchezo huo watafungiwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents