Habari

Ajali ya basi yaua wawili

Watu wawili wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa mkoani Ruvuma baada ya ajali ya basi aina ya Fuso yenye namba za usajili T 606 CTY ya kampuni ya Kisumapai linalofanya safari zake kati ya Songea, Mbinga na Nyasa.

Akithibitisha taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi amesema kuwa watu wawili wamefariki kwenye ajali hiyo iliyotokea ijumaa huku majeruhi wengine wakiwa wamepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu.

“Gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na dereva Ismail Mohamed Nasoro ilianguka na kupoteza maisha ya watu wawili hapo hapo, huku watu 42 wakiwa wamejeruhiwa mpaka sasa jumla ya majeruhi 33 kati yao walipata matibabu na kuhurusiwa na wengine 9 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga, Mbuyura” amesema Kamanda Gemini.

Baadhi ya majeruhi wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva pamoja na kubeba abiria kupita kiasi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents