Burudani

Album mpya ya ‘Touch My Blood’ yamrudisha rapa AKA kwenye ramani ya muziki

Album mpya ya ‘Touch My Blood’ ya rapa AKA kutoka Afrika Kusini imemrudisha rapa huyo kwenye ramani ya muziki nchini humo baada ya kupokelewa vizuri na kuweka rekodi kwenye mauzo.

Rapa AKA ambaye kwa miaka miwili mfululizo hajafanya vizuri kwenye muziki nchini humo, kupitia album yake hiyo  tayari amegonga mauzo ya Platnumz yaani kauza zaidi ya kopi laki 5 kwa mfumo wa nakala ngumu (hard copy).

Kufuatia mauzo hayo AKA jana amekadhiwa Plaque ya dhahabu na kampuni ya NYCE & Beam Group na album hiyo imeuza nakala zote hizo ndani ya siku 7 tangu iingie sokoni.

AKA kupitia ukurasa wake wa Instagram amewashukuru watu wote waliosaidiana naye kuandaa album hiyo pamoja na familia yake.

  • akaworldwide#TouchMyBlood 🔴📀 Thank You so much for the support … so many people said we couldn’t do it on our own. We went and found our own distributor, did our own marketing … shit, we even put up our own billboards. WE WENT GOLD IN A WEEK 📀 There were people who even tried to get this album pulled down, there were people who tried to use lawyers, said we would flop, said we weren’t experienced enough to do it … people who told us they made AKA. All they did was lie to themselves. YOU made AKA. Not even AKA made AKA. This is a small step on the way to Platinum 💿 for this CLASSIC ALBUM. (This GOLD award is purely based on HARD COPY SALES WE HAVENT COUNTED DIGITAL SALES AT ALL 💻📲🎹🎼) … Thank You to NYCE Entertainment & all the @beamgroup_GANG ❤️ … Thank GOD for giving me the strength & patience to pull this off with my friends and family. Thank You to all the artists who featured and producers who lent their talents to this project. We’ll get your plaques to you as soon as we can. #TouchMyBlood 🔴

Album ya Touch My Blood imeingia sokoni tarehe 25 mwezi Juni 2018 na imehusisha wasanii kibao kutoka Afrika Kusini akiwemo Yanga Chief na Kwesta na ina jumla ya nyimbo 16.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents