Burudani

Alikiba ajibu ombi la Diamond Platnumz ‘nipo tayari kudhamini Wasafi Festival kupitia Mofaya’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba amemjibu Diamond Platnumz kuhusu maombi yake ya kumuomba atumbuize kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Alikiba kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba amesema kuwa kwa sasa yupo bize kusambaza bidhaa za Mo Faya katika nchi mbalimbali, hivyo hatoshiriki kwenye tamasha hilo, lakini yupo tayari kuwa mdhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya.

Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.

Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrinkili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa. 

Jumatatu ya wiki hii, kwenye uzinduzi wa Tamasha la Wasafi Festival, Diamond alikaririwa akisema “nitafurahi kumuona kaka yangu Alikiba kwenye Wasafi Festival” huku akiahidi kuwa ataongea na uongozi wake juu ya maombi hayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents