Burudani

Aliyekuwa meneja wa Harmonize, Mr Puaz ashambuliwa kisa kauli ya ‘pesa imem-badili tabia Harmonize’

Aliyekuwa meneja wa Harmonize, Mr Puaz amejikuta akishambuliwa mtandaoni na mashabiki wa muimbaji huyo baada ya kueleza kwamba ameachana na msanii huyo baada ya pesa kumbadili tabia.

Meneja huyo alidai wakati akianza kazi na Harmonize alikuwa ni kijana mstaarabu lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga, mwanamuziki huyo aliyekiri kuwa anajituma alianza kubadilika suala alilodai kuwa huenda ni kutokana na mafanikio aliyoyapata na kwamba hana kinyongo naye na wala nia ya kumchafua.

”Naelewa kwamba ni kijana mdogo ambaye ametoka katika familia masikini, lakini utajiri na umaarufu aliopata kutokana na mafanikio ya muziki wake umeathiri tabia yake.

Mashabiki katika mitandao ya kijamii, wameanza kumshambulia meneja huyo huku wakienda mbali zaidi kumtaka aeleza sababu zilizomfanya aondoke wa muimbaji huyo. Haya ni maoni ya mashabiki.

Adolf Rafael

Hana kinyongo naye na wala hana nia ya kumchafua” Anaamini kuwa Harmonize ni kijana mdogo aliyetoka kwenye familia masikini. Kwa maelezo hayo huwezi kusema kuwa huna kinyongo naye.Halafu Harmonze naye akijibu mapigo utasemaje? Wabongo utawajua tu!

Shomari Selemani Manyengu 

Huwezi kumsimamia mtu mpaka kwenye mambo yake ya kibinafsi ww upo kwa ajili ya kumsimamia kwenye shughuli za ki music na sio kwenye mambo yake mengine hapo ni lazima mtashindwana tu.

Paul Komb

Kijana kahaso nakumbuka kuanzia kipindi kile anaosha magari pale mtwara kwa hiyo hata kama saizii anaringa mwache aringe kwa hiyo hapo meneja pambana na hali yako.

Gwamaka Pondo 

Watu wanafkiiii sana konde boy alipokuwa kwao mtwara mlikuwa hamumfuatilii kapata mshiko mmeanza shobo tangu lini Tanzania mtuakiwa maskini akipata utaskia analinga huyoo kabadilika.

Fabiano Luis

 Huna kinyongo wkt unatema nyongo?…vinginevyo ungejifunza kwa katibu wa timu fulani cjui afrika lion cjui nn amejiuzulu kistaarabu media zikamchokonoa lkn hakutema nyongo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents