Habari

Aliyekuwa rais wa Brazil Michel Temer atiwa mbaroni kwa tuhuma za Ufisadi (+ Video)

Rais Mstaafu wa Brazil, Michel Temer ametiwa mbaroni jijini Sao Paulo kwa tuhuma za rushwa na ufisadi.

Mstaafu huyo alitiwa mbaroni baada ya kinga aliyokuwa nayo ya kutoweza kushtakiwa akiwa Rais anayehudumu kuisha ambapo alikuwa Rais toka mwaka 2016 mpaka 2018.
Mara baada ya kuondoka madarakani ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikali walianza uchunguzi wa tuhuma za rushwa na ufisadi dhidi yake kupitia Operesheni ‘Car Wash’ dhidi ya viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi nchini Brazil ili kusafisha na kutokomeza ufisadi na rushwa.

Marais wastaafu wawili waliopita wa Brazil pia wamekumbwa na operesheni Car Wash kutokana na matumizi mabaya ya madaraka wakiwa ofisini na hivyo kutuhumiwa kuendekeza ufisadi na rushwa.

Panelli alisema hakimu huyo angeweza kuamua kuweka Temer chini ya kukamatwa kwa nyumba au aina nyingine ya ulinzi. “Aina hii ya kukamatwa hutokea tu wakati kuna hatari ya haraka mtuhumiwa anaweza kukimbia au kwamba bado anafanya uhalifu,” aliongeza. “Nina uhakika wanasheria wa [Temer] watatoa ombi la habeas corpus ili aweze kuendelea kujibu kwa mamlaka huru,”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents