Habari

Amuua mama yake kisa mtoto wa mbwa

By  | Polisi mjini Michigan – Marekani wanamshikiria kijana Andrew David Willson(19) kwa kosa la kumuua mama yake mzazi Lisa Marie Willson(51).

Baada ya kumkamata kijana huyo siku ya Ijumaa na kumfikisha mahakamani siku ya Jumatatu, polisi wameeleza kuwa Andrwer alimpiga risasi moja ya kichwa mama yake huyo aliyekutwa akitandani baada ya kumtupa nje mtoto wa mbwa aliyompeleka nyumbani kwao.

Licha ya kuwa mahakama ilimkuta kijana huyo na kosa la mauaji ila, polisi wamedai kuwa walipokea simu majira ya asubuhi kutoka kwa kijana huyo akidai kuwa amerudi nyumbani na amemkuta mama ameuwawa.

Akitoa ushahidi mahakanani mpelelezi wa makosa Charles Buckland, amesemea kuwa ni kijana huyo na mama ndiyo walikuwa nyumbani usiku wa tukio. ” Andrew Willson  aliongea na mama  usiku wa Alhamisi kuhusiana na kumpeleka mbwa huyo kwa baba yake,” amesma mpelelezi.

Akaongeza kuwa “Ilipofika usiku wa manane kijana huyo alichukua bunduki yenye risasi 22 na akaenda chumbani kwa mama yake  akafyatulia kichwani wakati mama yake huyo akiwa amelala.”

Chanzo: USA Today

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments