Habari

Atakayetupa takataka barabarani Dar, Kupigishwa deki

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda ametangaza kuwa kuanzia leo Julai 29, 2019 mtu yeyote atakayetupa taka taka barabarani achukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kushushwa kwenye gari na kufanyishwa usafi.

RC Makonda wa pili kutoka kushoto.

RC Makonda amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya usafi kwa jiji hilo ikiwa ni kipindi cha maandalizi wa ugeni wa viongozi takribani 16 kutoka nchi wanachama wa SADC kwa ajili ya mkutano Mkuu wa 38 wa SADC.

Ule utaratibu wetu wa Lugalo tunauanza leo, Kwenye barabara zote ndani ya mkoa wa Dar Es Salaam, Haiwezekani mtu uwe na nidhamu kwenye kile kipande cha karibia mita 200- 300 halafu hiyo nidhamu akifika kwingine inapotea. Kwa hiyo utaratibu wa mtu mwenye gari anakayetupa taka barabarani kuanzia leo mshusheni. Wekeni utaratibu mzuri, Akikataa kusimama chukueni Plate number yake toeni taarifa, Huyo mtu tutamkamata aje kufanya usafi kwa kupiga deki,“amesema RC Makonda.

Aidha, RC Makonda amewataka watu wanaoingia katikati ya Jiji ambao huwa na desturi ya kutooga asubuhi basi wapumzike majumbani kwa kipindi cha mwezi Agosti ili kuweka mazingira safi katika kipindi cha ugeni mzito wa viongozi wa SADC.

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaotazamiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Mbali na agenda nyingine za mkutano huo, Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  atapokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC kutoka kwa Rais wa Namibia, Hage Geingog.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents