Burudani

Avuliwa taji la U-Miss kwa kufananisha damu yake ya hedhi na watu waliokufa kwenye machafuko

Mshindi wa taji la ulimbwende nchini Uturuki 2017,  Itir Esen amepokonywa taji hilo siku mbili baada ya kukabidhiwa kutokana na mojawapo ya machapisho yake ya mtandao wa Twitter akifananisha damu ya hedhi yake na damu ya watu waliokufa kwenye machafuko ya jaribio la mapinduzi nchini humo mwaka jana.

Aliyevuliwa U-Miss Uturuki 2017, Itir Esen .

Kwenye moja ya Tweets zake, Itir Esen (18) alifananisha tukio la jaribio la mapinduzi mwaka jana nchini Uturuki lililoua watu takribani 300 kuwa damu yao iliyomwagika na yeye anasherehekea kwa kuvuja damu ili kuwaenzi.

Nimepata hedhi yangu asubuhi ya leo kusherehekea watu waliopoteza maisha yao mnamo tarehe 15 mwezi Julai, Ninasherehekea siku hiyo kwa kuvuja damu ya watu waliopoteza maisha yao.“ameandika Itir Esen kwenye moja ya Tweets zake.

Waandalizi wa mashindano hayo wamesema kuwa chapisho hilo halikubaliki na kuthibitisha uamuzi wao wa kumpokonya taji hilo saa chache tu baada ya kupata ushindi.

Tweet hiyo ilichapishwa wakati wa maadhimisho ya mapinduzi hayo mnamo tarehe 16 mwezi Julai wakati ambapo takriban watu 250 walifariki wakikabiliana na jaribio hilo la mapinduzi lililotekelezwa na upande mmoja wa jeshi.

Hata hivyo tukio hilo sio la kwanza nchini humo kwani mwaka 2016, mshindi mwingine wa taji hilo la mwaka 2006, Bi Merve Buyuksarac alipewa hukumu ya jela ya miezi 14 na kupokonywa taji kwa kumtusi Rais wa Uturuki, Reccep Tayyip Erdogan katika shahiri la kejeli alilolichapisha katika mtandao wa Twitter.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa akiwaita ‘mashahidi’ watu wote waliokufa wakati wa mapinduzi hayo.

Waandaji wa shindano hilo wanasema kuwa hawakuliona chapisho hilo hadi baada ya shindano hilo siku ya Alhamisi ya tarehe 21 Septemba mjini Instabul ambapo walifanya mkutano kujadili kabla ya kuapata uamuzi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents