Tupo Nawe

Baada ya kuugua Dengue: Babu Tale asimulia alivyolichungulia kaburi, Aamua kurudi Moro kusaidia wasanii kila Tarafa

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka kwa mara ya kwanza na kueleza jinsi alivyoteswa na ugonjwa wa Dengue wiki mbili zilizopita.

Picha ya Babu Tale kipindi alivyolazwa.

Babu Tale kupitia kipindi hicho chote alichougua, Amesema kuwa alikuwa anawaza endapo akifariki Kijijini kwake watamkumbuka kwa lipi? hivyo kwa vile amepona ameona ni vyema akarudi Morogoro na kuanza kusaidia wasanii wachanga kama kulipa fadhila kwa jamii.

Narudi nyumbani, Wiki iliyopita niliugua homa ya dengue. Nashkuru Mungu sasa ni mzima wa afya ila cha moto nimekiona. Katika suala hilo la kuumwa nimejifunza kitu. Watu walizusha nimekufa, niliwaza sana juu ya hilo. Niliwaza msiba wangu na yatakayoendelea baada ya mimi kufa. Nimejiona kabisa nikizikwa pembeni ya kaburi la baba yangu, kijijini nilikotokea ambako huwa nakwenda mara kwa mara kufagilia kaburi la baba.“amesema Babu Tale na kueleza namna atakavyowasaidia wasanii mkoani Morogoro.

Najua nimefanya mengi kwenye tasnia ya burudani hasa muziki wa bongo fleva. Ila nimewaza nyumbani nitaacha nini? Nimefanya mengi kwa watanzania wanaotoka maeneo mbalimbali, ila wadogo zangu wa nyumbani nimewafanyia nini? Hapo ndipo nilipoamua kuwafanyia kitu vijana wa nyumbani kwetu ninapotoka, kule nikatapozikwa.  Nimeamua kuwasaidia vijana wenye kipaji cha kuimba wanaotoka tarafa ya Ngengelele, Mkuyuni na Kiloka kwa kuchagua kijana mmoja kutoka kila tarafa. Hao vijana watatu nitawapa nafasi ya kurekodi wimbo na video kwa gharama zangu Na nitahakikisha wanatimiza japo ndoto zao za Sanaa.“amesema Babu Tale.

Wiki mbili zilizopita Babu Tale alishikwa na homa ya Dengue hadi kulazwa, Jambo ambalo lilipelekea mpaka kuzushiwa habari za kifo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW