Burudani

Baada ya mzozo wa jina la simba, Afande Sele atoa salamu za kheri kwa Diamond

Baada ya mzozo mkubwa wa kipindi cha nyuma wa kugombea uhalali wa umiliki wa jina la Simba kati ya mkongwe wa muziki wa Hip Hop, Afande Sele na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Hatimaye Afande Sele ameonekana kukubali yaishe kwani amemtakia kila la kheri Diamond kwenye uwakilishi wake kwenye Kombe la Dunia.

Tokeo la picha la afande sele
Afande Sele

Afande Sele amesema kuwa maendeleo hayana u-team hivyo anaamini kuwa kitendo cha Diamond kushiriki kwenye wimbo rasmi wa Kombe la Dunia ni jambo la kupongezwa na kila mtu.

Maendeleo hayana timu, kutoka Tandale hadi Rusia, Kinesi Cup hadi World Cup. Hongera sana mdogo wangu baba yake Tipha…Lion Never loose..💪…All the best Nasib/Tanzania.“ameandika Afande Sele kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Soma zaidi – Afande Sele kumaliza kesi ya neno ‘Simba’ kati ya Diamond na Mr Blue kwa style hii

Salamu hizo za Afande Sele zimekuja ikiwa ni siku tano zimepita tangu wimbo rasmi wa Kombe la dunia ‘Colours’ uliowakutanisha Jason Derulo na Diamond Platnumz.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents