Burudani

Baada ya Rihanna kutangaza kumburuza Mahakamani baba yake mzazi, Hatimaye mzee wake amjibu

Baada ya msanii wa muziki nchini Marekani, Rihanna Fenty kutangaza kuwa atamshtaki baba yake mzazi kwa kutumia jina la Fenty kibiashara, Hatimaye baba yake mzazi, Mzee Ronald Fenty amemjibu mtoto wake kuwa asijisumbue kwani jina hilo ameanza kutumia hata kabla ya yeye kuzaliwa.

Rihanna na mzazi wake Ronald Fenty

Mzee Fenty amesema alianza kutumia jina la Fenty kwenye  biashara zake kabla hata ya kumzaa Rihanna, Hivyo madai ya mtoto wake kuwa anamuharibia biashara yake ni ya kupuuzwa.

Ni miaka mingi nimekuwa nikitumia jina la Fenty kwenye biashara zangu hata kabla ya yeye *Rihanna* kuzaliwa. Madai yake kuwa najinufaisha na jina la ukoo la Fenty nimeyashangaa. Nafikiri kwa kuwa jina lake limekuwa kubwa duniani hivyo anafikiri yeye ndiye wa kwanza kutumia jina hilo, ukweli ni kwamba hapana nimeanza kutumia jina hilo kibiashara muda mrefu sana.“amesema  Baba yake Rihanna, Ronald Fenty juzi Juni 19, 2019 baada ya kutoka mahakamani kuomba shtaka hilo lifutwe.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeeleza kuwa Mzee Fenty anatarajia kufungua kampuni ya Fenty Entertainment, Jambo ambalo Rihanna anahofia kuwa kampuni hiyo itakuwa haraka endapo atatumia jina la Fenty.

Kwasasa Rihanna anatumia jina la Fenty kwenye bidhaa zake za vipodozi, Ambazo ni moja ya vitu vinavyomuingizia mkwanja mrefu zaidi ukitoa muziki.

Soma zaidi chanzo – https://theblast.com/c/rihanna-dad-lawsuit-reality-show-dismiss-fenty

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents