Habari

Benki ya NMB yatoa misaada ya mamilioni Mufindi, Kilolo, Arusha na Rorya mashuleni (Picha)

Benki ya NMB yatoa misaada ya mamilioni Mufindi, Kilolo, Arusha na Rorya mashuleni (Picha)

Benki ya NMB imeweza kutoa misaada ya viti na madawati katika shule mbalimbali nchini Tanzania kwa lengo la kuwezesha vijana wengi wa Kitanzania kupata Elimu bora kwa ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari.

Baadhi ya maeneoa ambayo Benki hiyo ilitoa misaada ni pamoja na MUFINDI, KILOLO, ARUSHA NA RORYA.

 

MUFINDI

Wanafunzi wa shule ya Msingi Maduma iliyoko Kata ya Maduma Wilayani Mufindi wakishangilia madawati waliyokabidhiwa na benki ya NMB juzi shuleni kwao.

KILOLO

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kihaka wilayani Kilolo – Iringa wakiwa wamebeba stuli za maabara muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NMB.Benki ya NMB ilikabidhi meza na stuli 60 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.

ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha – Mrisho Gambo(kushoto) akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo ya jijini Arusha wakati wa hafla ya kukabidhiwa meza na viti vyenye thamani ya shilingi 10 milioni vilivyotolewa na benki ya NMB. Katikati ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini – Aikansia Muro.

RORYA

Mkuu wa Wilaya ya Rorya – Simon Chacha akiwa ameketi na wanafunzi wa shule ya Msingi Minigo juzi (Jumanne) katika moja ya madawati yaliyotolewa na benki ya NMB ili kusadia kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo. Wengine ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (Mwenye koti na Tai Nyeusi) – Amos Mubusi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents