Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Beyoncé alirudisha kundi la Destiny’s Child kwenye tamasha la Coachella, Wizkid ashindwa kutumbuiza

Baada ya mwaka jana msanii wa muziki nchini Marekani, Beyonce kushindwa kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la muziki nchini humo la Coachella kutokana na ujauzito aliokuwa nao kipindi hicho, Hatimaye mrembo huyo asubuhi ya leo amefanya show ya historia kwenye jukwaa la tamasha hilo akiwa na memba wenzake wa Destiny’s Child.

Beyonce akiwa jukwaani

Beyonce ambaye alipanda na wasanii wenzake wa kundi la Destiny’s Child, Michelle Williams na Kelly Rowland walitumbuiza nyimbo zao kama  Say my name na Bills, Bills, Bills. Nyimbo ambazo ziliibua shangwe na baadaye Beyonce kuanza kutumbuiza na madensa wake.

Beyonce katikati akiwa na wenzake wa kundi la Destiny’s Child

Beyonce hajawakuna mashabiki pekee bali hata wasanii wengine wakubwa nchini humo kama Chance The Rapper naye amempigia saluti Beyonce kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa show kali aliyofanya.

Hata hivyo, huenda sasa hivi stori zingekuwa nyingine kama kama rapa pekee aliyechaguliwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo maarufu zaidi Marekani, Wizkid angefanikiwa kupanda jukwaani.

Waandaaji wa tamasha hilo jana walitoa taarifa kuwa rapa huyo amekwama kuingia nchini Marekani na kuahidi mashabiki wa Tamasha hilo kuwa atatumbuiza wikiendi ijayo.

Tamasha la Coachela linafanyika Indio, California na limeanza Ijumaa ya tarehe 13 Aprili na litamalizika Jumapili ya tarehe 15 Aprili 2018, Na limehudhuriwa na zaidi ya wasanii 120 wa muziki wa kimataifa.

Tazama video ya Beyonce alivyokinukisha Jukwaani;

https://youtu.be/jD4BHaWL1_I

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW