Habari

Bobi Wine atua Marekani kwa ajili ya matibabu, aahidi kulivua nguo jeshi la polisi nchini Uganda

Msanii wa muziki nchini Uganda na Mbunge wa jimbo la Kyadondo, Bobi Wine usiku wa kuamkia leo Jumapili Septemba 2, 2018 amewasili nchini Marekani kwa ajili ya kufanyiwa matibabu baada ya kupigwa na jeshi la polisi wiki mbili zilizopita.

Bobi Wine mwenye magongo

Akitoa ujumbe mzito baada ya kuwasili nchini Marekani, Bobi Wine ameahidi kuanika maovu yote aliyofanyiwa na jeshi la polisi ikiwemo kuteswa na kupigwa hadi kupelekea majeraha makubwa kwenye mwili wake.

Nimewasili salama nchini Marekani kwa ajili ya matibabu maalumu kufuatia manyanyaso na kipigo kizito nilichopata nikiwa mikononi mwa jeshi la polisi. Tunawashukuru watu wote duniani waliokuwa na sisi kwa kipindi chote, naahidi mapema nitatoa taarifa rasmi kitu gani kilichonitokea tangu nikamatwe Agosti 13, 2018.“ameandika Bobi Wine kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Bobi Wine mnamo tarehe 13 mwezi uliopita, alikamatwa na jeshi la polisi nchini Uganda kwa kosa la kuchochea vurugu na kumiliki silaha kinyume na sheria, kosa ambalo baadae aliachiwa huru na Mahakama ya Jeshi nchini humo.

SOMA ZAIDI – Bobi Wine aachiwa kwa dhamana, arudi uraiani akitembea na magongo

Related Articles

11 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents