Habari

Boomplay kuboresha tasnia ya muziki nchini Tanzania, yatangaza kushirikiana zaidi na wasanii wa Tanzania

Boomplay, App inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki, yafanya forum yake ya kwanza kwa ajili ya wasanii nchini Tanzania.

Katika forum hiyo, Meneja wa Boomplay Tanzania Bi Natasha Stambuli alizungumza kuhusu kuwezesha wasanii na uzalishaji wa muziki (Production) na usambazaji wa muziki kidigitali (Digital Distribution).

Meneja wa Boomplay Tanzania Bi Natasha Stambuli

Boomplay tunatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii kama kupata muda wa studio, ku-shoot video zenye quality ya kimataifa na mengine mengi. Tumeingia mkataba na Wanene Entertainment ili kuwezesha wasanii na matatizo hayo. Barani Afrika Boomplay ina ofisi Tanzania pamoja na Kenya, Nigeria na Ghana. Moja kati ya fursa zinazopatikana ni sisi kuwa na uwezo wa kujenga madaraja kwa wasanii wetu wa Tanzania na wasanii wengine kutoka nchi hizo” aliendelea Bi Natasha Stambuli.

Forum hiyo ilijumuisha jopo la wataalamu mbalimbali katika tasnia ya muziki akiwemo Bi Martha Huro – Meneja wa Boomplay Kenya, Lupakisyo Mwambinga – Mkuu wa Idara Ya Sheria COSOTA, Nahreel kutoka Navy Kenzo, Moses Range – Muanzilishi DEMO Innovators, Japhet Kapinga – Meneja Maudhui Boomplay na kuratibiwa na msanii wa miondoko ya Hip Hop, Wakazi.

Wasanii na watayarishaji pia walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa wataalamu hao na kupata ujuzi zaidi katika masuala ya sheria, hati miliki, branding na vingine vingi katika tasnia ya muziki.

Kuhusu Boomplay

Boomplay (ambayo awali ilikuwa ikifahamika kama Boomplayer), ni jukwaa linalotoa huduma ya kusikiliza na kupakua (download) muziki ambayo ipo chini ya umiliki wa kampuni ya Transsnet Music Limited.

Malengo ya app hii ni kutengeneza jukwaa kubwa na la kutegemewa na wasanii na wazalishaji wa muziki katika usambazaji wa kazi hizo za sanaa. Kwa sasa Boomplay ndio application kubwa na inayokuwa kwa kasi sana barani Afrika, ikiwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5.

Watumiaji wake wanaweza kusikiliza na kuangalia video bure, kwa kujisajili (subscribe) kupitia vifurushi vya siku,wiki au vile vya mwezi ambapo ambavyo vinawawezesha kuhifadhi (save) nyimbo offline au kununua nyimbo. Huduma hiyo kwa sasa inapatikana Android, iOS na wavuti.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents