Habari

BREAKING: Wema Sepetu ahukumiwa jela mwaka mmoja

Wema Sepetu ahukumiwa Jela mwaka mmoja au kulipa faini ya milioni 2

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya milioni 2 baada ya kukutwa na makosa mawili ya kutumia na kuhifadhi dawa za kulevya aina ya Bangi nyumbani kwake.

Wema Sepetu

Akisomewa hukumu hiyo leo Julai 20, 2018 katika Makahama ya Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, Wema Sepetu ametakiwa kulipa faini hiyo na kama akishindwa basi atapelekwa jela kutumikia adhabu hiyo.

Katika hukumu nyingine wafanyakazi wawili wa ndani wa msanii huyo ambao nao walitajwa kwenye kesi hiyo wameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kukutwa bila hatia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents