Habari

BRELA yataja viambatanisho muhimu wakati wa kufanya maombi leseni ya kiwanda

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetaja viambatanisho muhimu vinne ambavyo mtu anayehitaji kufanya maombi ya leseni ya kiwanda au cheti cha usajili anapaswa kuwa navyo.

BRELA imesema viambatanisho hivyo ni pamoja na hati za usajili wa mmiliki wa kiwanda, mchanganuo au andiko linalohusu kiwanda husika, uthibitishi wa eneo kilipo kiwanda pamoja na kibali cha. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Hayo yamebainishwa leo mkoani Morogoro na Mkurugenzi wa Leseni BRELA, Andrew Mkapa wakati akiwasilisha mada kuhusu utoaji wa keseni za biahara kundi A katika mafunzo ya sikuu nne ambayo yameandaliwa na BRELA.

Mkapa amesema kupitia kiambatanisho cha uthibitisho wa eneo kilipo kiwanda mtu anapaswa kuonesha mkataba wa pango, hati ya umiliki wa ardhi au barua kutoka kwa ofisa mipang miji.

“Vambatanisho ni utambulisho wa mmiliki ambapo atatakiwa kuwa na nyaraka au hati mbalimbali ambazo zinaelezea eneo husika’’’’’’ ambalo kiwanda kitakuwepo,uwezo wake kimtaji kwa maana ya uwekezaji na hivyo vyote vitaonekana kupitia andiko na nyaraka nyingine ambazo zitakuwa zimetolewa na taasisi nyingine.

“Lakini kiuhalisia viwanda vingi vinachafua mazingira inaweza isiwe papo kwa papo au kwa muda mrefu, ndio maana tunawaona Nemc ambao ndiyo wanaweza kutudhibitishia sisi kuwa eneo fulani hakuna uchafuzi wa mazingira,” amesema

Aidha amesema viwanda vimegawanyika katika makundi mawili kwa mujibu wa Sheria ambapo kundi la kwanza ni viwanda vikubwa na vya kati ambavyo mtaji wake unaanzia Sh.Milioni 100 na kundi la pili linahusisha viwanda vidogo ambavyo mtaji wake uko chini ya Sh.Milioni tano.

Amefafanua ada ya usajili wa leseni ya kiwanda ni Sh.800,000 na ada hiyo inalipwa mara moja tu kwa uhai wa maisha yote ya kiwanda lakini kwa upande wa viwanda vidogo ada ya usajili ni Sh.10,000 na hiyo ni kwa muda wote.

“Leseni ya viwanda vikubwa ni Sh.800,000, kiwanda ambacho uwekezaji wake hauzidi Sh.Milioni ni sh 10,000, uwekezaji ambao unazidi Sh.milioni tano ada yake ni Sh 50,000 na uwekezaji unaozidi Sh.milioni 10 ada yake ni Sh.100,000,”amesema Mkapa

Akifafanua zaidi Mkapa amesema kuwa baada ya kiwanda kupewa leseni au kusajiliwa kila mwaka wahusika wanatakiwa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kiwanda ambapo kuna fomu maalum ya kujaza ambayo inauliza maendeleo ya kiwanda.

“Na hii ripoti ya kiwanda ambayo inatakiwa kuwasilisha BRELA kila mwaka haina malipo katika kiwanda ni bure kama ukitoa taarifa ndani ya mwaka lakini ukichelewa ndio kuna faini ndogo kama Sh.10,000.

“Lakini tunaamanisha wenye Viwanda ambao wamepata leseni kutoa taarifa zao kwani zinasaidia kutunza kumbukumbu ambazo zinaweza kutumia na Serikali,”amesema

Hata hivyo amesema kuwa BRELA wameweka mkakati wao kwamba huduma yoyote ambayo watalifanya haitazidi siku tatu na kama ombi litakuwa limekamilika na hakuna maombi mengi kwa siku hiyo hata saa moja au mbili zinatosha kukamilisha huduma.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents