Habari

BUKOBA: Watu wawili wapoteza maisha na wengine watano kujeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa visu – Video

BUKOBA: Watu wawili wapoteza maisha na wengine watano kujeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa visu - Video

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya kuchomwa kwa kisu sehemu mbalimbali za miili yao, huku mmoja anayedaiwa kuwawachoma visu watu hao, akidaiwa kupigwa na wananchi, katika kituo kikuu cha mabasi manispaa ya Bukoba.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa Bukoba Dk. Mussa Sweya amekiri kupokea maiti mbili na majeruhi watano, na kuwa majeruhi wawili wametibiwa na kuruhusiwa kutokana na kuwa na majeraha madogo.

Pia amesema kuwa majeruhi watatu wamelazwa, na mmoja amefanyiwa upasuaji mkubwa, kutokana na kuathirika zaidi na majeraha hayo ya visu.

Mzazi wa mmoja wa majeruhi Athuman Mujuni ameeleza alivyopata taarifa za mtoto wake kuchomwa visu na kumkuta utumbo ukiwa nje.

Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa wameanza uchunguzi ili kubaini chanzo.

Chanzo Eatv.Tv.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents