Burudani ya Michezo Live

Burna Boy na baba yake wakatwa na polisi, Ighalo wa Man United atetewa na majirani – Video

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria  Damini Ebunoluwa Ogulu alimaarufu Burna Boy ameripotiwa kukamatwa na polisi mara baada ya majirani zake kutoa taarifa za malalamiko kwamba msanii huyo anafungulia muziki kwa sauti ya juu kiasi cha kusababisha kelele mtaani.

Mtandao wa Pulse Nigeria umeripoti kwamba Wananchi hao wenye hasira walifika nyumbani kwa staa huyo wakiwa na polisi huku wakitoa maneno kwamba imekuwa kero kwao, huku wakimtolea mfano jirani yao mwingine anayeishi katika Kitongoji au mtaa ule ule mchezaji wa Manchester United Odion Ighalo ambaye wanasema ni mtulivu na asiye na kelele za muziki nyumbani kwake.

Kwenye video zilizonaswa na Blog ya Linda Ikeji, Jirani mwingine alisikika akisema, Burna anapiga kelele hizo za muziki nyumbani kwake wakati bado anadaiwa hela ya kiwanja alichojenga Jumba lake hilo.

Mbali na yeye kukamatwa imeripotiwa kuwa Baba yake mzazi naye amekamatwa pia.

View this post on Instagram

#BURUDANI: Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria  Damini Ebunoluwa Ogulu alimaarufu Burna Boy ameripotiwa kukamatwa na polisi mara baada ya majirani zake kutoa taarifa za malalamiko kwamba msanii huyo anafungulia muziki kwa sauti ya juu kiasi cha kusababisha kelele mtaani. Mtandao wa Pulse Nigeria umeripoti kwamba Wananchi hao wenye hasira walifika nyumbani kwa staa huyo wakiwa na polisi huku wakitoa maneno kwamba imekuwa kero kwao, huku wakimtolea mfano jirani yao mwingine anayeishi katika Kitongoji au mtaa ule ule mchezaji wa Manchester United Odion Ighalo ambaye wanasema ni mtulivu na asiye na kelele za muziki nyumbani kwake. Kwenye video zilizonaswa na Blog ya Linda Ikeji, Jirani mwingine alisikika akisema, Burna anapiga kelele hizo za muziki nyumbani kwake wakati bado anadaiwa hela ya kiwanja alichojenga Jumba lake hilo. Mbali na yeye kukamatwa imeripotiwa kuwa Baba yake mzazi naye amekamatwa pia.

A post shared by bongo5.com (@bongofive) on

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW