Aisee DSTV!

Cardi B, French Montana na Yo Gotti kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za wizi

Rapper Cardi B, French Montana na Yo Gotti wameshtakiwa na DJ mkongwe nchini Marekani aitwaye,  DJ JMK kwa tuhuma za kutumia beat lake bila ruhusa yake.

DJ JMK amesema kuwa ameshafungua kesi kwa mastaa hao, Akidai kuwa French Montana na Yo Got, Cardi B na City Girls walitumia beat lake lililotumika kwenye wimbo “Choppa Style” ulioimbwa na Choppa kwenye nyimbo zao za “Oh Yeah” na “Twerk”.

DJ huyo amesema kuwa awali alishafanya mawasiliano na mastaa hao, Na waliahidi kuwa watamlipa lakini mpaka sasa hawajamlipa.

DJ huyo amesema kuwa yeye ndiye aliyetengeneza beat hilo mwaka 2000 na alikuwa analitumia kwenye klabu, Kabla ya kumruhusu Choppa kutumia beat hilo kwenye wimbo wake wa “Choppa Style”.

Wimbo wa Choppa Style ulitoka mwaka 2002 na upo kwenye album ya ‘Straight From The N.O” ya rapper Choppa. Kwasasa wimbo huo umetazamwa mara milioni 9 kwenye mtandao wa YouTube.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW