Habari

CCM yadai CHADEMA hawawezi kutatua kero za wananchi

Wakazi wa Kata ya Moita, wilayani Monduli mkoani Arusha wameombwa kumchagua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wapate maendeleo na kuachana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwani hakiwezi kutatua matatizo yao kwenye jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaban Mdoe wakati akizungumza kwenye kampeni eneo la Moita Bwawani mkoani Arusha.

Msidanganywe na Chadema, hawawezi kutatua kero zenu, alikuwepo diwani wao, hadi amejiuzulu, mbunge wa zamani Lowassa hivi sasa hawezi tena kuwasaidia.” amesema Mdoe wakati akimnadi mgombea udiwani wa CCM kwenye kata hiyo, Ndugu Prosper Meyani.

Kauli hiyo ya Mdoe imekuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu Waziri Mkuu Mstaafu wa zamani, Edward Lowassa kuzindua kampeni katika kata hiyo na kuwataka wananchi kuchagua kiongozi kutoka CHADEMA.

Awali, aliyekuwa diwani wa kata hiyo kupitia tiketi ya CHADEMA ambaye alijiuzulu, Edward Sapunyo alisema aliamua kujiuzulu baada ya kunyimwa ushirikiano na madiwani wa chama hicho na kuamua kurudi CCM alikotokea.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Sapunyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli kupitia CCM, alisema chaguo sahihi katika kata hiyo ni mgombea wa CCM.

Halmashauri ya Monduli hadi sasa inaongozwa na CHADEMA kutokana na kuwa na madiwani 18 na CCM madiwani tisa pekee, Uchaguzi mdogo wa Madiwani wa kata 43 nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.

Chanzo:Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents