Habari

CHADEMA ‘watema cheche’ baada ya Mbunge wao kuhamia CCM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimetoa tamko lao rasmi leo desemba 14, 2017, ikiwa ni masaa machache yaliyopita baada ya aliyekuwa Mbunge wa wa Jimbo la Siha, Dkt. Godwin Oloyce Mollel kupitia tiketi ya chama hicho kujivua Ubunge.

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema

Chadema wamesema wameshangazwa na sababu za Mhe. Mollel kujivua nafasi hiyo ya Ubunge kwani hazina mashiko.

“Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa. Sababu hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi. Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu.”Imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande mwingine CHADEMA imetoa ushauri kwa Viongozi wake wote wanaotaka kuhamia CCM kuwa wajifunze kutoa sababu za msingi na sio kuwahadaha wapiga kura wao kwa ajili ya matumbo yao.

Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya ‘hapa kazi tu’ na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.

Hili linakuwa pigo lingine kubwa kwa CHADEMA kuondokewa na Mbunge wao na kukimbilia CCM ikiwa ni wiki mbili tu zimepita tangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa hama hicho, Patrobas Katambi kutangaza kuhamia CCM.

Soma taarifa kamili kwa vyombo vya habari kutoka CHADEMA;

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) . TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) leo tarehe 14 Disemba,2017 tumepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Siha Dr.Godwin Mollel amejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM .
Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa.

Sababu hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.

Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu.
Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya ‘hapa kazi tu’ na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.

CHADEMA tuko imara sana na tutaendelea na ajenda zetu bila kuyumbishwa na wimbi hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga kura wao kwa kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali kwa maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.

Tutaendelea kujenga Taifa letu na Chama chetu bila kujali njaa za baadhi yetu wala maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama. Ni dhahiri wale waliotanguliza ubinafsi hatutaweza kufika nao mwisho wa safari hii.

Imetolewa leo Alhamis 14 Novemba, 2017

JOHN MREMA-Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents