Aisee DSTV!

DAR: Abiria afariki dunia ndani ya Basi Ubungo, Yaelezwa alikuwa ni msafiri wa Tabora

Abiria mmoja aliyetambulika kwa majina ya Mwanaidi Said (83), aliyekuwa anasafiri kutoka Dar Es Salaaam kwenda mkoani Tabora, amefariki dunia jana alfajiri katika kituo cha mabasi cha Ubungo akiwa ndani ya  basi kabla ya kuanza kwa safari.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Mussa Taibu amesema kuwa abiria huyo amekutwa na mauti akiwa amekaa kwenye kiti cha basi hilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kigoma kupitia mkoani Tabora.

Kamanda Taibu amesema Msafiri huyo “Alikuwa akisumbuliwa na saratani na alikuwa anakwenda mkoani Tabora baada ya kumaliza matibabu yake hapa Dar es Salaam na vyeti vimeonyesha hivyo,“.

Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto wa mama huyo aliyekuwa ameambatana naye kwenye safari hiyo, Faida Paul amesema kuwa mazishi ya mama yake yamefanyika jana Kigamboni.

Chanzo: https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Abiria-afia-ndani-ya-basi-stendi-ya-Ubungo/1597296-5168498-6vv8n8/index.html

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW