Burudani

Davido aweka rekodi nchini Uingereza katika uwanja wa ‎‎O2 Arena, ala sahani moja na Drake, Beyonce na Kanye West (+video)

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido usiku wa kuakia leo ameweka rekodi ya kuwa msanii mdogo kiumri kutoka Afrika kujaza uwanja maarufu wa matamasha ya muziki wa The O2 Arena uliopo jijini London nchini Uingereza.

Davido kupitia show hiyo, ambayo alikuwa peke yake, amefanikiwa kuuza tiketi 20,000 ambazo ndio idadi ya watu wanaoingia kwenye uwanja huo.

Kwa matokeo hayo, Davido anakuwa ni msanii wa pili kutoka Afrika kujaza uwanja huo, hii ni baada ya Wizkid mwaka jana naye kufanya hivyo.

Wasanii wengine wa kimataifa ambao walishawahi kujaza uwanja huo ni
Beyoncé, Rihanna, Kanye West, Drake, Elton John Prince, Alicia Keys, Adele, Celine Dion, Britney Spears . Tazama show yake hapa chini

https://youtu.be/-huj_S1x1tY?list=RD-huj_S1x1tY

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents