Habari

Dawa ya nguvu za kike kuingizwa sokoni mwezi Septemba mwaka huu, Yadaiwa itawasaidia kufika kileleni ndani ya dakika 4

Shirika la udhibiti wa chakula na dawa nchini Marekani (FDA), limetoa dawa maalumu aina ya Vyleese ya kutatua na kutibu tatizo la ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Dawa ya Vyleesi

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), dawa hiyo itaanza kupatikana katika baadhi ya maduka ya dawa nchini humo kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa dawa hiyo itarudisha hisia kwa wanawake waliokosa hisia za mapenzi na imetengenezwa na Kampuni ya Palatin Technologies na kuruhusiwa kuuzwa na maduka ya Amag Pharmaceuticals.

Imeelezwa kuwa dawa hiyo hutumika kupitia sindano ambayo husisimua neva inayotumika katika hisia za kushiriki tendo la ndoa. Vilevile ilisema ukosefu wa hisia husababishwa na mwanamke kutoshiriki vizuri katika tendo la ndoa.

Kemikali kwa jina la Vyleese imejaribiwa kutengeneza kile ambacho kinaweza kuitwa viagra ya kike. Hili ni suala tata kwa baadhi ya wataalamu wanahoji asili ya tatizo la hisia za kingono na kukosa ukosefu wa msisimko wa mapema wakati muathirika anapotumia.” Imeeleza taarifa.

Aidha taarifa hiyo, imeeleza kuwa dawa hiyo itarudisha hisia kwa wanawake na huenda mtumiaji akafikia kileleni ndani ya dakika 4-7 endapo ataitumia vizuri.

Je, tatizo hili lipoje kwa hapa Tanzania? Akizungumzia sababu zinazosababisha wanawake wakose hisia za tendo la ndoa nchini, Daktari wa wanawake kutoka Hospitali ya Palestina – Sinza, Dar es Salaam, Dkt. Ali Njama, amesema tatizo kubwa linasababishwa na msongo wa mawazo na maradhi.

Sababu kubwa ni msongo wa mawazo, kuna vitu anakuwa amevishikilia moyoni ambavyo labda alikwazwa na mpenzi wake, anakuwa hana furaha, labda kwa ugumu wa maisha. Nyingine ni maradhi, ugomvi wa mara kwa mara na mpenzi wake, hivyo zote hizo na nyingine zinamfanya akose hamu ya kufanya tendo la ndoa,” amesema Dkt. Njama kwenye mahojiano yake na gazeti la Mtanzania.

Nae Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dkt. Muzdalfat Abeid, amesema hakuna tafiti zozote zilizofanyika kuthibitisha tatizo hilo kama lipo au laah..

Chanzo: http://mtanzania.co.tz/dawa-nguvu-za-kike-sokoni-septemba-madaktari-wazungumzia-ukubwa-wa-tatizo-nchini/

Soma zaidi- https://www.fda.gov/news-events/press-announcements/fda-approves-new-treatment-hypoactive-sexual-desire-disorder-premenopausal-women

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents