DC Hai Ole Sabaya, ashangazwa na wanafunzi wa kiume kulala kitanda kimoja, hamjui madhara yake ? (+Video)

Serikali wilayani Hai Imetoa masaa 24 kwa Shule ya Sekondari patmo kuhakikisha wanafunzi wa kiume wanaolala wawili katika kitanda kimoja huku wakichangishwa Tsh laki nane na nusu kwa ajili ya malezi kwa kila mwanafunzi wanapatiwa malazi haraka sana vinginevyo atalazimika kuchukua hatua kali.

Mkuu wa wilaya ya Hai @lengai_ole_sabaya amewaonya wamikili wa shule hiyo kufuatia kitendo cha kuanzisha bweni huku wakiwa hawana kibali na katika hilo kuwapa mwezi mmoja kukipata vinginevyo shule hiyo itakuwa imejifunga kwa kutoza wanafunzi fedha nyingi na kushindwa kutoa huduma za msingi.

Huku akiwaonya wadhibiti ubora na maafisa elimu kwa kushindwa kufanya wajibu wao wa msingi wa ukaguzi badala yake kuhangaika na masauala binafsi ya waalimu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW