Habari

Diamond aumizwa na wingi wa kodi TRA (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameonesha kuvurugwa na wingi wa makato ya kodi anazotozwa kwenye matamasha yake ya Wasafi Festival na show zake nyingine za ndani.

Diamond akiongea na maafisa TRA mkoani Iringa, Aliwauliza bei ya kubandika bango (Posters) yenye ukubwa wa A4 ni shilingi ngapi?.

TRA walimjibu Diamond kwa kusema kuwa, Viwango vya bei za Posters inategemea na ukubwa wa bango lenyewe na eneo husika kwa kutumia ‘By Law’ zinzotumika eneo hilo.

Diamond aliendelea kuhoji kuhusu bei ya mabango hayo kwa kutoa mfano, Ambapo alisema kuwa mwaka huu walienda kupiga show Kahama mkoani Shinyanga na walipoenda kufuatilia bei za kupandika mabango (Posters) aliambiwa na TRA wilayani humo kuwa kila bango litatozwa Tsh elfu 3 kwa siku.

Diamond aliendelea kuhoji kwa kuuliza, “Kwa mfano sisi kama Wasafi Limited kila mwisho wa mwaka tunalipa kodi zetu sawia kabisa. Na miongoni mwa shughuli nyingine tunazozifanya ni pamoja na kuandaa show za Wasafi Festival. Je, unatakiwa ulipe kodi ya mwisho wa mwaka au nilipe pale pale 18% ninapomaliza show ambayo tumeandaa sisi wenyewe.?”

TRA wamemwambia kuwa kama tamasha limeandaliwa na Wasafi Limited, Hawezi kukatwa 18% palepale baada ya show kumalizika na badala yake, Kinachotakiwa ni yeye kutunza nyaraka zote za malipo na gharama zote zilizotumika na kodi atakatwa mwishoni wa mwaka  kama kampuni nyingine zinavyokatwa.

TRA wamesema kodi ambazo angeliweza kutozwa ni zile ambazo labda show yake imedhaminiwa na kampuni nyingine hapo angeweza kutozwa kodi ya zuio.

Diamond amesema kuwa kuna baadhi ya Mikoa TRA walikuwa wanamkata asilimia 18 pale pale baada ya show, Halafu tena mwisho wa mwaka wanamkata tena kodi nyingine ya Kampuni. Ile hali show zote zimeandaliwa na Wasafi Limited.

Kwa mujibu wa maelezo yao, Mfano wa mikoa ambayo show zilizoandaliwa na Wasafi Limited na kukatwa asilimia 18 pale pale ni Geita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents