Burudani

Diamond na Mameneja wake waweka wazi sakata la Rich Mavoko kuondoka WCB (+video)

Uongozi wa WCB leo Agosti 14, 2018 umeweka wazi kuwa ni kweli Rich Mavoko ana matatizo na lebo hiyo kubwa barani Afrika na tayari mambo yote yameshapelekwa BASATA na wanatarajia kukaa kikao na Baraza hilo na baada ya hapo BASATA watatangaza rasmi maafikiano yatakayopatikana.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa WCB, Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema kwa sasa asingeliweza kuzungumzia kila kitu kwani ishu hiyo ipo BASATA ila wataongea rasmi baada ya maafikiano.

Wiki iliyopita Rich Mavoko alienda BASATA kulalamika kuwa mkataba wake na WCB unamnyonya na kulitaka Baraza hilo kuupitia upya.

Related Articles

11 Comments

  1. Waongee nae tu wakubaliane upya maana @Rich Mavoko ni msanii mzuri na kipaji anacho ila akiimba peke ake peke ake hata hasikiki.Kwa mfano pindi hajasign WCB alitoaga ngoma inaitwa Pacha Wangu ila haikuwika na zipo ngoma kibao nyuma ya hiyo nzuri ila hazikuhit lakini alivo sign WCB akatoa Ibaki Story kuna watu ndo wakamfaham na kuanza kumfatilia wakidhani ni upcoming artist wakati ni mkongwe.!!! Kwa hiyo yeye mwenyewe atulize akili kisha afanye uamzi sahihi hasije jikuta baadae anajutia uamzi wake.

    #WCB_The_house_of_Hits.

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents