Diamond Platnumz atangaza habari njema kwa mashabiki wa WCB

Diamond Platnumz atangaza habari njema kwa mashabiki wa WCB

Diamond Platnumz akiwa na watoto wake Tiffah na Nillan

Kama wewe ni shabiki wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz au pengine unawakubali wasanii wengine wa kutoka WCB  basi habari hii ikufikie.

Habari njema ni kwamba mwezi ujao mwezi Agosti 06, 2018 ndio mwezi ambao mtoto wa kwanza wa Diamond Platnumz, Tiffah anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na Diamond ameahidi kusherehekea kitofauti kidogo ambapo amesema kuwa atawaalika mashabiki wake 30 kwenye Party hiyo itakayofanyika Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond amesema kuwa mashabiki hao atawalipia gharama zote za nauli kwenda na kurudi na huduma za malazi.

Watu 30 Wenye Bahati ntawalipia Ndege na Malazi kwenda Kusheherekea na @princess_tiffah Uzaliwa wake South Africa….. wanyumbani kama kawa LIVE on @wasafitv“ameandika Diamond.

Party hiyo pia itarushwa live kupitia kituo chake cha runinga cha Wasafi TV na itaambatana na Birthday Party ya Romy Jons.

Hata hivyo, haijaelezwa ni njia zipi atatumia kuwapata mashabiki hao 30 lakini mashabiki wake endeleeni kumfuatilia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwani huko ndiko atakakotangaza vigezo na masharti.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW