Habari

DPP wa Kenya Noordin Haji aeleza sababu za kumkamata Gavana wa Nairobi Mike Sonko – Video

DPP wa Kenya Noordin Haji aeleza sababu za kumkamata Gavana wa Nairobi Mike Sonko - Video

Polisi nchini Kenya imemkamata Gavana wa jimbo la Nairobi Mike Sonko, kwa tuhuma za ufisadi. Hii ni baada ya mkurugenzi wa mashataka ya umma nchini Kenya, Nurdin Hajj kutoa agizo la kukamatwa kwake kwa madai ya kuhusika kutoweka kwa dola milioni 3.5 za umma.

Bwana Sonko ni gavana wa tatu aliyepo mamlakani kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi.

Gavana Sonko alikamatwa siku ya Ijumaa katika mji wa Voi pwani ya Kenya saa kadhaa baada ya Mkurugenzi wa mashitaka ya umma kusema kuwa ana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka mwanasiasa huyo.

Gavana huyo akihutubu wakati wa sherehe ya kupanda miti 12 Mei eneo shule ya Moi Forces, Mathare jijini NairobiGavana huyo akihutubu wakati wa sherehe ya kupanda miti 12 Mei eneo shule ya Moi Forces, Mathare jijini Nairobi

Bwana Sonko anatuhumiwa kwa kutoa zabuni kwa washirika wake wa karibu, kugushi nyaraka na ubadhirifu wa wa fedha za jimbo la Nairobi.

https://www.instagram.com/p/B5vmmoCh4Ea/

Sonko alivyokamatwa na polisi.

https://www.instagram.com/p/B5vS1VNBJ9h/

Mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya umma pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu madai ya gavana huyu kuingilia kati uchunguzi kwa kujaribu kuficha ushahidi.

Awali Sonko aliwasilisha kesi mahakamani kuomba uchunguzi dhidi yake ukomeshwe lakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali. Gavana huyo pia alidaiwa kukabiliwa na tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji wa fedha. Hivi karibuni mamlaka ya magereza ilimtuhumu kwa kutoroka jela miaka 20 ilkiyopita.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents