Habari

Fahamu mambo matatu ambayo wakazi wa Dar hawatakiwi kufanya katika kipindi hiki cha mkutano wa SADC

Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) mwaka huu unafanyika Tanzania Jijini Dar Es Salaam  na tayari umeshaanza juzi tarehe 05 August 2019 na utaendelea hadi tarehe 18 August 2019.

Dar Es Salaam

Mkutano huo utahudhuriwa na wakuu wa nchi 16 na wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa afrika (SADC).

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limejipanga kikamilifu kuhakikisha amani na utulivu vinatawala katika kipindi chote cha mkutano huo, Na kupiga marufuku mambo makubwa matatu kwa wakazi wa Jijini la Dar Es Salaam mpaka mkutano huo utakapomalizika.

1-Marufuku kuweka taa za vimulimuli, Taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye Magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki zote za kiraia, isipokuwa magari yanayotoa huduma za dharura tu na ya makampuni binafsi ya Ulinzi.

2-Marufuku pikipiki (Bodaboda ) zote kuingia katikati ya Jiji kuanzia tarehe 06 August hadi 18 August, 2019. Kutokana na sababu ya baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepiga marufuku bodaboda kufika maeneo yote ya katikati ya Jiji.

3-Marufuku kuingilia misafara ya wageni, wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu kipindi hiki cha ugeni mkubwa wa kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents