Habari

Fatma Karume amburuza mahakamani Mwanaharakati Cyprian Musiba

Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amemshtaki Cyprian Musiba katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa madai ya kukashifiwa na mwanaharakati huyo.

Fatma Karume

Akizungumzia shtaka hilo, Fatma Karume amedai kuwa wanatakiwa kufika katika mahakamani Oktoba 3 mwaka huu, Kwa ajili ya kutajwa kwa kesi hiyo Na. 39 ya mwaka 2019.

Ninamshtaki kwa kunikashfu kwa kusema kwamba eti nimetiwa mimba na muuza unga, na kwamba sina staha, mimi nina mume na watoto, sasa siwezi kukubali ujinga huu,“ameeleza Fatma kwenye mahojiano yake na gazeti la Nipashe.

Fatma ambaye pia ni wakili wa kujitegemea, anaungana na Waziri wa zamani Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kufungua mashtaka kwa madai ya kushushwa hadhi na Musiba.

Mwanaharakati huyo ambaye amekuwa akijipambanua kuitetea serikali, amekuwa akiingia katika migogoro na watu mbalimbali ikiwamo hivi karibuni kuingia katika vita ya maneno na Waziri wa Mambo ya Ndani na Nchi, Kangi Lugola, baada ya waziri huyo kumtaka kutofautisha harakati zake na serikali.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents