BurudaniUncategorized

Hamisa Mobetto na Vera Sidika wavimbiana

Mavideo vixer matata kutoka Afrika Mashariki, Vera Sidika wa nchini Kenya na Hamisa Mobetto kutoka Tanzania, wamerushinana maneno kisa video ya Snapchat.

Hamisa ambaye bado yupo nchini Kenya, alitumia mtandao wa Snapchat kujirekodi video akiwa na rafiki kipenzi wa Zari The Boss Lady, baada ya video hiyo kusambaa na kuzua minong’ono ikiwemo maswali ya kwani Vera amegombana na Zari? Hii ni kutokana kuwa binti huyo amekuwa akituhumiwa kutaka kiharibu mahusiano ya kimapenzi kati ya Diamond na Zari.

Kutokana na hali hivyo Vera ameibuka na kuanza kutoa utetezi wake kwa madai kuwa, mrembo wa Tanzania alirekodi video pasipo yeye kujua na wala hakupanga kukutana naye kama inavyodaiwa.

Snapchat za Vera Sidika:

Vera akaongeza kwanza hamjui Hamisa ila alipokea ujumbe kutoka kwa binti huyo akimuomba wakutana kwani anampenda, kufuatia utetezi huo wa Vera, Hamisa amedai kuwa mtembo huyo wa Kenya ni muongo kwani alikuwa akijia kama anarekodiwa na wala hakumtafuta kuonana naye.

Snapchat za Hamisa Mobetto:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents