DStv Inogilee!

Hii ndio taasisi inayotoa huduma ya matibabu bure jijini Dar

Taasisi ya Mkono wa Tumaini inayofanya kazi za kusaidia jamii kwa kutoa huduma za matibabu bure maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, imeweza kuendelea la jukumu la kusaidia jamii ya watu wa Kinondoni hasa maeneo ya Kinondoni shamba na maeneo ya jirani kuwasaidia kupata unafuu kwa matibabu wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za kuwaona madaktari.

10995988_1437850883176131_1662728636697019795_n
Baadhi ya wananchi wa Kinondoni wakisubiri kupewa huduma na waataalam wa taasiso hiyo

Taasisi hiyo, inayofanya kazi chini ya kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church Kinondoni, imekuwa ikifanya kambi ya matibabu bure mara nne kwa mwaka ili kuwawezesha wananchi kuweza kupata matibabu na msaada wa kisheria na ushauri nasaha, ushauri wa kisheria na kibiashara bila malipo yoyote.

11139375_1437850826509470_6536097231515405168_n

Madaktari na manesi hujitolea bure kwasababu taasisi hii haifanyi kazi za biashara, inategemea zaidi michango ya waumini na watu mbalimbali ambao wanaweza kujitolea kusaidia jamii ndio maana watu wenye taaluma za udaktari, manesi, watu wa maabara, wanasheria na wataalamu wa biashara hujitoa kwa muda wao kuweza kuwashauri watu wa jamii ya Kinondoni.

“Hakuna anayelipwa kwenye taasisi hii, kila mtu anafanya kazi kwa kujitolea na malengo ni kufikia watu wengi zaidi kwa kuwapatia huduma za matibabu bure ili afya za watanzania ziweze kuimarika hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kifedha kuwaona madaktari na hawawezi kununua dawa,” anasema mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bi Annabela Munyagi.

Ukiondoa matibabu, watu vile vile waliweza kupatiwa nguo pamoja na chakula hii ni kutokana na kwamba wananchi wengi wanaoishi Kinondoni, wanaishi kwenye mazingira magumu hasa wazee na wajane ambao kipato chao ni cha hali ya chini sana.

Kupatiwa angalau chakula cha kumsaidia siku mbili au moja si haba kuweza kupunguza makali ya utafutaji kwa watu hawa.

Bi Munyagi alitoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa kusaidia watu wasiojiweza ili kupunguza makali ya maisha kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Kama kila mtu ataweza kuwa na uwezo wa kujitolea kusaidia watu, jamii yetu itapunguza matatizo mengi na hivyo kuachana na dhana ya kusubiri serikali ifanye wakati sisi kama wananchi wenyewe tunaweza kusaidia watu wanaotuzunguka kama tukiamua kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW