Habari

Hii ndio tathmini ya miaka miwili ya utawala wa Rais Magufuli

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbasi

Ni miaka miwili sasa imepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli aingie madarakani tarehe 5 Novemba mwaka 2015. ambapo mpaka sasa kuna mambo mengi ameyafanya ambayo ni moja ya sehemu za ahadi zake alizoahidi alipokuwa akijinadi kwenye kampeni mwaka 2015.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jumapili  jijini Dar es salaam, Msemaji Mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema ndani ya miaka miwili mengi yametekelezeka ambapo ametoa tathmini katika maeneo 10 muhimu.

HII NDIO TATHMINI YA UTAWALA WA RAIS MAGUFULI NDANI YA MIAKA MIWILI YA UONGOZI WAKE.

1-Dkt Abbasi amesema uwajibikaji wa watumishi wa umma na wananchi kwa jumla umekuwa mkubwa kwa kuwa kumekuwepo na ari ya kufanya kazi.

Tunajivunia kuongezeka kwa ari na nidhamu kwa watumishi wa umma.“amesema Dkt. Abbasi.

2- Dkt Abbasi amesema ni msukumo ambao Serikali imeweka katika ukusanyaji wa kodi na kinachopatikana kinatumika ipasavyo.

Zaidi ya Sh236 bilioni ziliokolewa kutoka kwa walipa kodi zilizokuwa zinawalipa watumishi hewa, tumeondoa watumishi wenye vyeti feki. Zaidi ya Sh142 bilioni nazo zimeokolewa kutoka kwa watumishi walioghushi vyeti na zote zimeelekezwa kutatua kero za wananchi,“-Dkt Abbasi.

3- Dkt Abbasi amesema vita ya ufisadi imekuwa kubwa na imesaidia kuleta mageuzi na fedha ambazo zimekuwa zikiokolewa kutokana na vita hiyo zinaelekezwa kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo.

Kuna Mahakama ya mafisadi imeanzishwa, kesi zake zinaanzia ngazi ya chini na mpaka sasa kuna kesi tatu, mbili ziko Dar es Salaam na moja iko Mtwara na zingine 107 ziko ngazi za chini zinashughulikiwa,“-Dkt. Abbasi.

4- Dkt. Abbasi amesema kuwa “Serikali inavyopigania rasilimali za Taifa. Vita katika eneo la madini tumefanya kupitia upya mikataba na kubwa tumejitambua kama Taifa na sasa wawekezaji wanajua Tanzania ukienda lazima uheshimu sheria.

5- Dkt Abbasi amesema uamuzi mgumu lakini makini uliofanywa na Serikali ingawa wapo waliopinga na kueleza haiwezekani, lakini imewezekana.

“Watumishi kutokwenda nje ya nchi, kati ya mwaka 2014/15, Sh216 bilioni zilitumika lakini kwa miaka miwili hii ni Sh25 bilioni pekee ndizo zimetumika. Mimi nimesafiri mara mbili tu.

6- Dkt. Abbasi ametaja ni azma ya nchi kujitegemea akisema wananchi wanafanya kazi ili kutekeleza hilo. Amesema ukusanyaji mapato umeongezeka kutoka Sh9.9 trilioni hadi Sh14 kwa mwaka.

Makusanyo ya mwaka yameongezeka kutoka trilioni 9.9 mwaka 2015 hadi trilioni 14 mwaka 2017” – Dkt. Abbasi.

7- Dkt. Abbasi amesema miradi mikubwa inatekelezwa kama vile ujenzi wa reli ya kisasa na uboreshaji wa shirika la ndege, akisema ununuzi wa ndege umefanyika na  hadi Julai,2018 zitakuwa zimewasili nchini.

Kipande cha reli ya kisasa kinachojengwa kutoka Dar hadi Dom kitagharimu TZS Tril 7.1 ikiwa ni fedha za ndani”- Dkt. Abbasi.

8- Dkt Abbasi amesema Serikali imeongeza bajeti katika maeneo muhimu ya sekta za afya, elimu bure na miundombinu ya barabara.

Kumekuwepo na upatikanaji wa dawa katika hospitali zetu ukilinganisha na awali, hii inasaidiwa na mkakati wa Serikali wa kununua dawa moja kwa moja kwa wazalishaji na bajeti ya Wizara ya Afya imeongezeka kutoka Sh30 bilioni hadi Sh261 bilioni, yote haya ni mafanikio ya miaka miwili,

9- Dkt. Abbasi amesema ndani ya miaka miwili serikali ya Rais Magufuli imeondoa kodi zilizokuwa zinatozwa kwenye bidhaa za kilimo.

“Katika sekta ya kilimo tumeondoa Tozo na Kodi nyingi zilizokuwa kero kwa watanzania”-Dkt. Hassan Abbasi.

10- Dkt Abbasi amesema kuwa serikali imejitahidi kutatua kero ya umeme kwa kuongeza uzalishaji kwa kuongeza mitambo ya uzalishaji.

Mradi wa Kinyerezi 2 wa megawati 240 uko katika 84% kukamilika, mtambo wa 1 wa megawati 30 utawashwa Desemba,2017″-Dkt. Abbasi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents