Habari

Hivi ndivyo mvulana wa miaka 19 alivyopora mkoba kisha kumchoma kisu mwanafunzi wa Chuo cha KIU, Polisi wamkamata Dar (+Audio)

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata kijana Ernest Joseph (19) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala, Anifa Mgaya aliyefariki dunia Juni 17 baada ya kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Juni 19, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Madale na amekiri kufanya tukio hilo.

“Mtuhumiwa katika mahojiano na Jeshi la Polisi amekiri kumchoma kisu kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo huku akieleza namna mwanafunzi huyo alivyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio kuwa ni fulana nyeusi, suruali ya Jinsi na Kapelo nyeusi. “Aidha mtuhumiwa alikiri kumpora pochi iliyokuwa na simu moja aina ya Tecno rangi nyeusi, fedha taslimu Shilingi 8,000 na vitambulisho mbalimbali ambavyo alivitupa na simu hiyo kuiuza,”amesema Kamanda Mambosasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents