Burudani

Hizi ndio video 5 za muziki zilizotazamwa zaidi kwa muda wote kwenye mtandao wa YouTube barani Afrika

Watu wengi kwasasa hususani wadau na mashabiki wengi wa muziki duniani kote, Wamekuwa wakifuatilia video za nyimbo za wasanii wao wanaowapenda kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo mtandao wa YouTube.

Kwa hapa Afrika wasanii pia wamekuwa wakipata mashabiki wengi kutoka nje ya mipaka yao hii ni kutokana na nguvu ya mitandao ya kijamii. Na imesaidia pia nyimbo zao kupenya hata kwenye mataifa ambayo kwa kipindi cha nyuma ilikuwa ni ngumu muziki wao kuwafikia watu.

Je, Hapa Afrika ni video gani za muziki zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube ambao unaonekana kuwanufaisha zaidi wasanii hao?

Hapa chini tumekuletea orodha ya video 5 za muziki zilizotazamwa zaidi barani Afrika.

1-Video ya wimbo wa LM3ALLEM ulioimbwa na Saad Lamjarred. (Views Milioni 757).

Saad Lamjarred ni msanii wa muziki kutoka Morocco na wimbo wake wa LM3ALLEM ndio wimbo wa kiarabu uliotazamwa zaidi kwaenye mtandao wa YouTube. Video ya wimbo huo iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube mwaka 2015.

2- Video ya wimbo wa DÉCAPOTABLE wa Zouhair Bahaoui (Views Milioni 295).

Zouhair Bahaoui ni msanii wa muziki pia kutoka Morocco, Video ya wimbo huu iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube mwaka 2018.

3- Wimbo wa Magic In The Air ulioimbwa na kundi la Magic System kutoka Ivory Coast (Views Milioni 261).

Moja ya nyimbo ambazo zimetokea kupendwa zaidi kwa mashabiki wa mpira barani Afrika, Huu wimbo wa ‘Magic In The Air’ umekuwa ukichezwa kwenye viwanja mbalimbali vya mpira wa miguu nchini Ivory Cost na Ufaransa.

Video ya wimbo huo, Ilitoka mwaka 2014 na tayari imeshatazamwa mara milioni 261 kwenye mtandao wa YouTube.

4-Ghaltana na Saad Lamjarred (Views Milioni 239)

5-Video ya wimbo wa Baby’s On Fire (Views milioni 226)

Wimbo wa Baby’s On Fire umeimbwa na kundi maarufu la muziki nchini Afrika Kusini linaloitwa ‘DIE ANTWOORD’ na video ya wimbo huu ilitoka mwaka 2012.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents