Michezo

Hoteli waliofikia England kwa ajili ya EURO ni hatari (Video)

Timu ya Taifa ya England tayari wapo nchini Ujerumani kwa ajili ya michuano ya Euro 2024.

Wapo kundi C na Jumapili hii wanacheza na Serbia katika mchezo wa ufunguzi majira ya saa nne Usiku.

Hiyo sio Story bali story ni eneo walilofikia kwa ajili ya kupumzika wakiwa wanajiandaa na Michuano.

Eneo hilo linaitwa Weimarer Land Spa and Golf resort in Blankenhain lipo mbali kidogo ya mji waliofikia wa Jena Ujerumani ingawa michezo watachezea kwenye uwanja wa club ya Schalke 04 unaoitwa Arena AufSchalke uliopo kwenye mji wa Gelsenkirchen kaskazini mwa Ujerumani.

Umbali kati ya hii miji miwili, Jena ambapo ndio wamefikia na Gelsenkirchen ambapo ndio Uwanja watakaotumia kwa ajili ya michuano ni Kilometa 385.6 yaani mwendo wa masaa manne na dakika 25.

Ni sawa na kutoka Dar Es Salaam mpaka Mkoani Tanga, wao hawajali umbali wanajali sehemu nzuri ya Kufikia 😂 Wanacheza Mji tofauti na walipofikia.

Eneo hili la mazoezi linafanyika michuano na mashindano ya Golf Ujerumani, ni moja ya Hoteli Ya Kifahari zaidi.

Hawa jamaa Watoto wa Mfalme wanapenda kujitofautisha sana 😂

 

https://www.instagram.com/reel/C8IBHT6NcjI/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents