Habari

IGP Simon Sirro: Ni kweli magaidi 300 walivamia Kitaya mkoani Mtwara (+Video)

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro amesema magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji.

Vyombo vya habari vya ndani nchini humo kikiwemo Jamii Forums na Mwanahalisi Digital vinaripoti kuwa IGP Sirro ameeleza kuwa wahalifu hao waliowajeruhi vijana watano huku baadhi yao walitoraka na kuacha mitumbwi yao.

Inaelezwa kwamba baadhi ya washukiwa wa tukio hilo wamekamatwa na msako unaendelea.

“Ukifanya uhalifu Tanzania na damu ya Mtanzania haiwezi kwenda hivi. Tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa,” amenukuliwa Sirro akisema.

Aidha Bwana Sirro amewasihi vijana kutojiingiza kwenye uhalifu.

Awali, Tanzania ilipeleka vikosi vyake kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Msumbiji baada ya kuibuka kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na wanamgambo kutoka kaskazini mwa Msumbiji, wanamgambo ambao wamekuwapo tangu mwaka 2017.

https://www.instagram.com/tv/CGpRXXfh5ZL/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents