Habari

Je una ujuzi huu zaidi ya cheti chako?

Ni vigumu kujua ujuzi wa ndani ya mtu na ni upi wa muhimu zaidi. Hapa ninakupa vigezo vya muhimu pale mwajiri anavyozungumzia ujuzi mwingine ukiondoa vyeti vyako ulivyoonyesha. Na ujuzi huu ni wa muhimu sana ambao utakusaidia kujenga mahusiano mazuri na wafanya kazi wenzako au wewe kuwa msaada kwa watu wengine.

viavogue0a5c949172fddbaf8a7264cf2346c6aa

Mara nyingi vitu hivi havitiliwi mkazo kwenye mfumo wetu wa elimu, hivyo basi unahitaji kujifunza kila siku na kuhakikisha unapata ujuzi madhubuti ambao utaboresha mazingira yako ya kazi na kwa watu wengine wafurahie kufanya kazi na wewe;

1. Ujuzi wa kuwasiliana

Huu ujuzi ni muhimu sana kwa kila tangazo la kazi, mara nyingi huandikwa hivi (good communication skills). Watu wenye ujuzi huu ndio wanaoongoza kuwa na mahusiano mazuri na watu wengine popote pale. Husikiliza vizuri na kuwasiliana vizuri na watu wengine. Watu wa namna hii, wako makini hata kwenye maneno au maongezi wanayofanya hivyo kila mtu hupenda kuongea nao.

2. Ujuzi wa kufanya maamuzi

Kuthaminiwa na mwajiri kwa sababu nyingi tu inakupasa kujua kufanya maamuzi ni ni jambo la msingi sana ili uweze kuendelea kwenye maisha ya kila siku. Maisha ya kila siku yameambatana na maamuzi kila sehemu na kila wakati, mara nyingi maamuzi sahihi hayahitajiki sana, ila ulifanya maamuzi na ukaendelea mbele bila kujali yalikuwa sahihi au si sahihi.

Hivyo basi hata katika ajira watu wenye uwezo mzuri wa kufanya maamuzi yenye tija huwa wanahitajika sana, ni wepesi wa kufikiri, kuangalia faida na hasara ya maamuzi ambayo wanatakiwa kufanya na huweza kuja na maamuzi. Kwa lugha nyepesi ni kwamba huwa wanakuwa na majibu wakati wote jambo lolote linapotokea.

3. Kuwa na motisha kutoka moyoni

Watu wenye motisha ya kutoka ndani, huwa hawahitaji mtu kumsimamia kwa kuwa wao utendaji kwao ni kitu kinachotoka moyoni. Huu pia ni ujuzi ambao unahitaji mtu mwenye uelewa na anayeweza kutambua binafsi kitu gani kinapaswa kufanyika na kukifanya bila kusukumwa sukumwa.

4. Ujuzi wa kiuongozi

Huu ni ujuzi mwingine ambao tunategemea mtu mwenyewe auendeleze, kuna mafunzo mengi ya uongozi ambayo yapo tayari sehemu tofauti tofauti na makala nyingi za namna gani unaweza kuboresha na kukuza ujuzi huu. Kwenye makala zijazo tutaendelea kukuelekeza mbinu tofauti tofauti za kukuza uwezo wako wa kuongoza.

5. Ujuzi wa kufanya kazi na timu ya watu wengine au wafanyakazi wenzako

Ujuzi huu hauna tofauti na ujuzi wa kuongoza, ingawa hapa inajumuisha uwezo wako wa kuwasiliana sawasawa, uwezo wa kusikiliza vizuri na kuelewa na kuweza kutengeneza ripoti ambayo inasaidia timu nzima kusonga mbele.

6. Ubunifu na uwezo wa kutatua matatizo

Siku hivi ubunifu na uwezo wa kutatua matatizo vinahitajika sana ingawa ni vigumu sana kuendeleza ujuzi huu kwasababu ni nadra sana. Kuna watu wengi wanaamini watu wabunifu huzaliwa na hawatengenezwi na kuna wengine wanapata ujuzi huu kirahisi sana. Lakini jambo la msingi ni kwamba unaweza ukaendeleza ujuzi huu ukiweka juhudi katika kutafuta na kusoma kwa kufuatilia mambo mbalimbali unaweza kujikuta unajenga ubunifu ndani yako.

7. Uwezo wa kutunza na kufuata muda

Mtu mwingine anaweza kusema suala hili linaendana na tabia. Na kwa sababu tu ya uvivu hawawezi kufuata muda na kufanya kazi mpaka  kwa usimamizi wa hali ya juu. Lakini haujachelewa unaweza kubadilisha mwelekeo wa mambo yako na kuanza kufanya kazi kwa kuzingatia muda.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents