Habari

Jeshi la Magereza lafunguka tetesi za Lulu kuachiwa huru ‘bado ni mfungwa, hakutakuwa na upendeleo’

Jeshi la Magereza limetoa ufafanuzi juu ya tetesi za kuachiwa huru kwa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye inasemekana amemaliza hukumu ya kifungo chake cha nje.

Related image
Lulu katikati kwenye picha

Kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo, Amina Kavirondo, amesema kuwa muigizaji bado ni mfungwa kwani kuna utaratibu uliowekwa ambao atapaswa kuufuata ili aweze kuachiwa huru na Magereza.

Taratibu nafikiri zinaeleweka, (Lulu) anakuwa bado ni mfungwa, na anapokuwa na kifungo hicho cha nje kuna taratibu zake, akimaliza basi kuna taratibu kama mfungwa yeyote, hata kama ni maarufu. Kile ambacho Lulu atafanyiwa ndicho atakachofanyiwa mfungwa mwingine yeyote, ‘treatment’ yetu ni sawa na wafungwa wengine,“ameeleza Bi. Kavirondo kwenye mahojiano yake na mtandao wa kituo cha runinga cha EATV.

Kwa upande mwingine, Kavirondo ameeleza kuwa Lulu mwenyewe anajua taratibu za kufuata ili aweze kuachiwa huru “mwenyewe anajua anatakiwa afanye nini, yule ni mfungwa kama wengine, hawezi kumaliza akaondokea kule kule” .

Lulu mapema mwaka huu alihukumiwa miaka miwili Jela, kwa kosa la kuua bila kukusudia na baadae alibadilishiwa hukumu hiyo kutokana na msamaha wa Rais na kupewa kifungo cha nje, ambapo mwezi huu (Novemba) anatarajiwa kumaliza adhabu yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents