Habari

Jeshi la polisi latangaza kubadilisha sare zake, Sababu kubwa mbili zatajwa

Ni nadra sana kusikia jeshi la polisi kubadili sare zake lakini hii inawezekana kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na ujanja wa baadhi ya wahalifu ambapo kila kukicha wanazidi kuongezeka.

(DCP) Joseph Attah

Sasa nchini Nigeria Jeshi la Polisi-kikosi cha usalama barabarani wametangaza kuongeza aina nyingine ya sare ambayo itatumika kama mbadala kwa jeshi hilo.

Sare za awali

Akitoa taarifa hizo Jumanne ya Aprili 03, 2018. Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama barabarani nchini humo, (DCP) Joseph Attah alisema kuwa lengo la kubadilisha sare hizo ni kuendana na hali ya hewa na kuongeza usalama zaidi wa polisi wanavyokuwa kwenye maeneo ya kazi.

“Tunautangazia umma kuwa jeshi letu la polisi kitengo cha usalama barabarani limebadilisha sare zake ili kuendana na hali ya hewa. Tumekuwa tukiona polisi wetu wakiwa mabarabarani na wengine kwenye maeneo ya viwanja vya ndege wakitokwa na majasho kutokana na joto hivyo tumefanya hivyo na kwa kuanza tutaanza na wakuu wa vituo vyote nchini na baadaye jeshi lote,”Imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na DCP Attah kupitia ukurasa rasmi wa jeshi hilo wa facebook (https://www.facebook.com/customsng/) .

DCP Attah amesema sababu nyingine ni kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi kwa polisi wanapokuwa kwenye vtuo vya kazi kwani sare hizo zitawafanya wajione wakipekee kwa kubadilisha kila siku.

Hata hivyo, mpango huo wananchi wengi wa Nigeria wameipinga wengi wao wakidai kuwa ni mpango wa mke wa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, Asha Buhari kwani tenda hiyo haijatangazwa wazi na serikali haikuwa na mpango huo wa maboresho na hata kwenye bajeti ya wizara ya mambo ya ndani haikuanishwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Vanguard wa nchini Nigeria umeeleza kuwa mabadiliko hayo yatagharimu zaidi ya Naira bilioni 1 sawa na bilioni 6 za kitanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents