Habari

Kampuni ya Mohamed Dewij ya METL, yafutiwa umiliki wa mashamba 6 na Serikali

Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (Metl) imepata pigo baada ya kufutiwa umiliki wa mashaba sita na Serkali yenye ukubwa ekari 12,915.126 yaliyopo Korogwe jijini Tanga.

Uamuzi huo wa kufutiwa umiliki huo ulitangazwa jana na Naibu Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angeline Mabula mara baada ya kumaliza kutembelea mashamba hayo ya METL, kampuni ambyo inongozwa na mfanyabiashara mkubwa hapa nchini Mohammed Dewij, alimaarufu Mo Dewij.

Mashamba yaliyofutiwa kibali yako sita kati ya 14 yanayomilikiwa na kampuni hiyo na yaliyopo katika eneo la Mombo, Mabango pamoja na Kwalukonge huko wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Naibu waziri huyo alisema uamuzi huo umekuja baada ya ushauri uliotolewa na Halimashauri ya Wilaya ya Korogwe kutokana na kutoendelezwa kwa muda sasa na ili kuleta nidhamu kwa watu waliokabidhiwa rasilimali za Serikali kuzingatia masharti ya uwekezaji.

Mabula aliongeza mapendekezo hayo yaliwasilishwa kwa Rais Magufuli na Wizara ya ardhi ikafanya ufuatiliaji katikaHalimashauri husika, alisema baada ya kujiridhisha walirudisha mapendekezo wa Rais na kuridhia.

Aliongeza uamuzi huo wa Rais kuridhia unabatilisha mashaba 6 kati ya 14 yanayomilikiwa na Mohammed Enterprises na unalenga kuhakikisha kuwa wote walipewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti ya uwekezaji na taratibu za uwekezaji.

Naibu Waziri aliongeza kuwa mashamba yaliyobakia ambayo hayajafutiwa kibali yanawekewa utaratibu kwa nia ya kuboreshwa kwa kuwa baadhi yake yanahitaji maboresho ili yafanye kazi.

Na kuitaka Halimashauri ya wilaya ya Korogwe kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika eneo la mashamba yaliyofutwa na watakaopewa eneo katika mashamba hayo ni wananchi waliokuwa wakiishi katika mshamba hayo na sehemu iliyobaki atafutwa mwekezaji mwingine kwa kuwa lengo la Serikali ni kuwa na wawekezaji wa viwanda.

Mabula alimpongeza mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella kwa kufanya kazi nzuri ya kufuatilia na kusimamia maagizo mbali mbali tangu Mh. Rais alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa wake.

Baada ya hapo mkuu huyo wa mkoa aliongea na kuwataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba yaliyobatilishwa hadi hapo Halimashauri ya wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi katika mashamba hayo.

Alisema ndani ya wiki hii ataitisha mkutano na wataalamu wa sekta ya ardhi katika mkoa huo pamoja na wale wa bodi ya mkonge kuangalia matumizi ya ardhi iliyobatilishwa kwa wananchi.

Chanzo https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Serikali-yafuta-umiliki-mashamba-/1597296-4935344-b3x6srz/index.html

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents