Burudani

Kauli ya Drake yaleta gumzo, yaaminika ni dongo kwa Soulja Boy ‘Be you, do you’ (+ Video)

Rapper kutoka Canada, aliyehamishia makazi yake mitaa ya Hiden Hills California Aubrey Drake Graha alimaarufu Drake ameamua kuvunja ukimywa kuhusu tuhuma zake ambazo amekuwa akiziongelea Soulja Boy.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa P Diddy kuna clip fupi ya video inayomuonyesha Drake akiongea baadhi ya maneno yanasemekana kuwa ni dongo kwa Msanii mwenzake kutoka Marekani Soulja Boy.

Ikumbukwe kuwa Soulja Boy alizua gumzo siku kadhaa nyuma na kusema kuwa Drake ameiba staili yake ya kuimba, na kwenye clip hiyo Mkali P Diddy ameandika maneno haya


“Do YOU. Be YOU. Get OFF the Phones and Computers and GO DO SOMETHING!!!⁣⁣⁣
NOW I’M INSPIRED!! Thanks 
@champagnepapi ⁣⁣⁣( ambaye ni Drake)

Maana yake ikiwa ni ” Fanya chakwako, kuwa wewe, kaa mbali na simu na kompyuta nenda kafanye kazi “

Kwa maneno haya inaonesha kabisa ni dongo kwa Soulja Boy ambaye amekuwa akiitumia simu yake kuwaponda baadhi ya wasanii akiwemo Tyga, Kanye West na Drake.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents