Habari

Kila mtu ni wa pekee na wa tofauti mpe nafasi katika maamuzi yake

Wakati unapoendelea kuishi katika dunia hii, lazima ujue kwamba wewe ni nani na una makusudi gani katika maisha yako. Ingawa tumeishi katika dunia ambayo watu wengine ambao wanaweza kukwambia wewe ni nani na unapaswa kufanya nini.

woman-thinking

Si vibaya kuwa na watu wa jinsi hiyo, ila katika kipindi maalumu cha maisha yako na kwa makusudi sahihi, wakati wa kuzaliwa ulihitaji wazazi ili waweze kukulea na kuhakikisha unakuwa na kusimama na uweze kujitegemea katika maisha yako. Ndio maana katika nchi mbalimbali ukifikisha miaka 18 wewe si mtoto tena bali ni mtu mzima ambaye anaweza kufanya maamuzi yake bila kuingiliwa na mtu yeyote kama hajavunja sheria.

Ingawa hilo somo ni gumu kueleweka miongoni mwa watu wengi, na watu wengi hudhani wanatakiwa kutawala rika fulani la watu kwasababu ya umri wao na nafasi walionayo kwenye familia. Kila jambo lina wakati wake na lazima ifike mahali tutambue ya kuwa kama jamii ikishindwa kujenga msingi wa mtu au mtoto mpaka anafikisha miaka 18 ni sawa tu na usemi wa kiswahili unaosema “samaki mkunje angali mbichi” je tunajua ubichi wa vijana na watoto wetu uko mpaka wapi?

Hivyo turudi kwenye makala hii, “kila mtu ni wa pekee na tofauti” kwasababu hiyo ndio maana kila mtu akifikisha umri fulani hutamani kufanya kitu fulani ingawa wakati akiwa mdogo alilazimishwa kufanya kitu fulani na wazazi wake. Hapo ndipo watu wengi waliweza kupoteza mwelekeo wa maisha kwa kujaribu kumfurahisha mtu mwingine katika maisha yake binafsi.

Kitu cha msingi unatakiwa kujua utofauti wako na upekee wako uko kwenye nini na unatakiwa ufanye nini? Hapa haimaanishi uache kuheshimu watu wengine, hapana bali ujue namna ya kushughulika nao bila kuharibu kusudi la maisha yako.

Kila mtu ana ladha tofauti tofauti ya kitu fulani, hivyo usilazimishe ladha yako ndio iwe ladha ya mtu mwingine. Unachotakiwa tu ni kushauri kwa kumsaidia lakini si kwa kumfanyia maamuzi. Hebu jiulize siku haupo nani atafanya maamuzi yake? Na ukweli ni kwamba hautakuwepo wakati wote kwa ajili ya huyo mtu ila unahitaji kuwa mkweli na mwenye ushauri wa kusaidia wengine. Vile vile wewe ni nani anakufanyia maamuzi? Kama hakuna anayekufanyia maamuzi basi huna haki ya kumfanyia mtu maamuzi ila unapaswa kumshauri vizuri yeye abakie kuamua kinashoweza kumsaidia.

Ukijua ya kuwa kila mtu ni tofauti utagundua kuwa wengi tunaishi maisha ya watu wengine bila kujua au kwakujua au kwa kujaribu kuwaridhisha watu wengine bila kujari hatima yako itakuwaje?

Inakubidi utafute na kujua kitu gani kinaweza kufanya kazi kwenye maisha yako kwanza kabla watu wengine hawajakuwekea vitu vyao kwa ajiri ya faida zao wenyewe huku wakikuwekea mazingira kana kwamba na wewe unafaidika kumbe hamna kitu hicho ni kiini macho. Fungua macho yako uone! Je, wewe ni nani na una tofauti gani na wenzako na unapaswa kufanya nini?

Inawezekana kabisa tuko hapa tulipo wengi wetu kwasababu tunawafanyia watu wengine kazi au tunaishi maisha ya watu wengine hivyo hatujawahi kuishi maisha yetu na hata hatujui yanafananaje. Hii ni fikra ya hali ya juu ambayo inakuhitaji kuanza kufanya uchunguzi wa hapo ulipofika na je umefikaje? Je ni kitu ambacho kimo ndani yako au umepandikiziwa tu? Kama umepandikiziwa kulitokea nini?

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents