Habari

Kimbunga Irma kuendelea kutesa Amerika

Kimbunga cha Irma kwa sasa kinadaiwa kimeelekea  katika visiwa vya Turks na Caicos vilivyopo karibu na Uingereza baada ya kusababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean na kuwaua  watu takriban 14, hata hivyo inahofiwa huwenda kimbuka hicho kitafika hadi maeneo ya Bahamas.

Imelipotiwa kuwa visiwa vilivyo nyanda za chini vipo kwenye hatari kubwa zaidi ya kukubwa na uharibifu endapo kukawa na mawimbi ya kiwango kikubwa yenye urefu wa mita 6. Mpaka sasa watu milioni 1.2 wameathiriwa na kimbunga hicho na  huwenda idadi hiyo ikaongezeaka na ikawa kubwa zaidi.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kufika maeneo ya Cuba baada ya kupiga jimbo la Florida nchini Marekani mwishoni mwa wiki, na Mkuu wa shirika la huduma za dharura la Marekani amethibitisha kutokea kwa uharibifu mkubwa.

Kutokana na kuwepo kwa mafuriko makubwa katika sehemu mbalimbali ilimeripotiwa  kuwepo kwa  magonjwa ya mlipuko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents