Habari

“Kiongozi wa serikali yangu akikuomba rushwa mpige risasi, Nitajibu mimi mahakamani” – Rais Duterte

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amewaruhusu wananchi kumpiga risasi kiongozi yeyote wa serikali atakayewaomba rushwa.

 Rodrigo Duterte

Akihutubia mamia ya wananchi wiki iliyopita katika Jimbo la Bataan, Kaskazini mwa Jiji la Manila, Duterte amesema kuwa rushwa ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya taifa hilo.

Durtete amesema kuwa mwananchi yeyote anayemiliki silaha, Anamruhusu kumtwanga risasi kiongozi yeyote atakayeomba rushwa lakini sio kumuua bali kumjeruhi.

Kiongozi huyo anayetajwa kuwa ni Dikteta, Amesema kuwa mwananchi akimjeruhi kiongozi aliyeomba rushwa yeye atasimamia kesi yake mahakamani.

Kiongozi wa serikali yangu kama atakuomba rushwa, Mpige risasi ila usimuue wewe mjeruhi tu. Mimi najua hili taifa linakwamishwa na rushwa, Hivyo mkiwajeruhi hawawezi kurudia na mimi nitawafukuza serikalini. Narudia mwananchi unayemiliki bunduki, usimchekee kiongozi anayekuomba rushwa, Mimi nitakusimamia mahakamani na huwezi kufungwa.” amesema Duterte.

Rais Duterte ni moja ya viongozi duniani wanaotajwa kuvunja haki za binadamu kwa asilimia kubwa zaidi duniani. Hii ni baada ya mwaka juzi kufanya msako wa kuvunja magenge ya wahalifu na wauza madawa ya kulevya na kisha kuwaua.

Mwaka jana pia Rais Durtete aligonga vichwa vya habari duniani, Baada ya kumtukana Mwenyezi Mungu ‘Mpumbavu’ kwa kitendo cha kumuumba Eva na kumuweka na Adam katika bustani ya Edeni huku akiwakataza wasile tunda la katikati huku akijua kitu hicho hakiwezekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents