Burudani

Lupita Nyong’o atoa shavu kwa wanafunzi Kenya

Muigizaji wa Filamu mwenye asili ya nchini Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o ametoa shavu kwa wanafunzi 1,200 nchini Kenya.

Muigizaji huyo ametoa shavu hilo kwa wanafunzi waliopo Kisumu- Kenya, kuweza kuitazama filamu ya Black Panther amabyo ilitoka rasmi Ijumaa iliyopita ya tarehe 16.

Udhamini wa muigizaji huyo umekuja baada ya kuanzisha mashindano ya mtandao yaitayo #BlackPantherChallenge, yenye lengo la kusaidia watu wanaotamani kuitazama filamu hiyo ila kutokana na kushindwa kumudu gharama zake wanashindwa kuitazama.

“I joined the #BlackPantherChallenge and sponsored 1,200 schoolchildren to watch the film in Kisumu, Kenya with my mother’s help. I wanted kids from my hometown to see the positive images reflected in the film and superheroes that they can relate to on the big screen. No matter where you live, you can help make this happen for more children who can’t afford to see the movie,” ameandika Lupita kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kutoa msaada huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents