Burudani ya Michezo Live

Mabeste awaomba watu waache kumtukana yeye na aliyekuwa mke wake, Baada ya kuvunjika ndoa yao na kuweka ugomvi wao mitandaoni – Video

Mabeste awaomba watu waache kumtukana familia yake baada ya kuvunjika ndoa yao na kuweka ugomvi wao mitandaoni - Video

Mwanzilishi wa harakati za Piga Kambi Utalii wa Ndani, Lisa Karl Fickernscher ambaye alikuwa ni mke wa msanii wa Hip Pop hapa nchini Mabeste amefunguka kiundani kuhusu maisha yake na aliyekuwa mume wake.

Maisha ya wawili hao yalikuwa maarufu zaidi kupitia mtandao wa instagram ambapo watu wengi zaidi pasi kujua nyuma ya pazia ya maisha yao walikuwa wakifurahia familia yao na kutamani kuwa kama wao.

Ambapo Lisa kupitia Youtube chaneli ya simulizi na sauti amefunguka mazito ukweli kuhusu maisha ya mahusiano yao nje ya kile ambacho mashabiki wengi walikuwa wanakiona kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Ndoa si siri tena, juzi tumeyasikia ya Stamina kupitia sanaa yake leo Lisa amefunguka kinagaubaga sababu ambazo zimepelekea kuvunja ndoa yake na Mabeste na yapita mwaka sasa tangu wawili hao kufarakana.

Akihojiwa Lisa amehadithia sababu kuu mbili za kuachana na Mabeste ambapo ametaja kuwa Mabeste alikuwa mwanaume mwenye mkono mwepesi wa kumpiga hata mbele ya watoto wake , lakini pia ameeleza kuwa Mabeste hakuwa mwanaume wa kujitoa na mtafutaji kwaajili ya familia yake.

Pili amesema kwa asilimia 80 Mabeste alikuwa hasimamii majukumu yake kama baba wa familia na mume kwake.
”Hakuwahi kusimamia majukumu yake, sikuwahi kula hela ya muziki wake,… Kuna tofauti kubwa sana kati ya mkulima anayeenda shambani analima lakini hapati mavuno kuliko yule ambaye hafanyi kitu anashonda tu nyumbani…

Mabeste alikuwa mzito sana infika stage mnagombana nageuka kama mzazi kwake namlea kama navyolea watoto” amesema Lisa
Lisa ameongezea ”Alikuwa hataki kufanya chochote, kunipenda sio kusema unanipenda kunipenda ni matendo, sikuajiliwa, mwenzangu alirelax hakuwa na wivu mwanamke nimehudumia familia miezi miwili mitatu, alikuwa hata hajiulizi natoa wapi hakuwa na wivu”.

Aidha Mabeste na Lisa wameachana yapita mwaka sasa wakiwa na watoto wawili, Kendrick na Catelyn Mabeste.
Pia tumeona kumekuwa na mfumuko wa matukio ya aina hiyo ya ndoa za watu maarufu kufarakana jambo ambalo si jema sana kwani linatishia pakubwa sana wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa.

Baada ya hayo Mabeste pia aliongea ya kwake kuhusu ndoa hiyo kuvunjika, akiongea Clouds Tv Mabeste alifunguka mengi sana. huku akidai mwanamke huyo aliamua kumacha kisa hana pesa na kuamua kuchukuliwa na rafiki yake wa karibu sana.

Baad aya hayo yote Msanii huyo amewaomba Watanzania waache kumtukana yeye pamoja na aliyekuwa mke wake Lisa, kupitia ukurasa wake wa Instagram Mabeste amefunguka haya:-

“Guyz nawaomba Muwe Down Kabisa kwenye hili, Msinitukane wala Msimtukane Mzazi mwenzangu Coz Ukweli Haupo kamilifu ndani yenu katika kuamini hichi tunacho Zungumza .!! Bali kila Mmoja anahadisia tu Maisha yake yanyuma na Mwenza wake katika Alivyo mtenda kwa Ubaya Please nawaomba Mimi kama Mimi samahani 🙏 Coz Mimi sitaongelea Mapungufu ya Mwenza Wangu Kamwe, But kutokana na Maswali yenu juu ya Familia Yangu Yalikuwa Mengi,Na Mlishiliki katika Kutu Support juu ya Kuumwa kwake so Nikajaribu Kuongelea Kwa Nini Tulitengana Tu ..!! Na TATIZO NI CHITTING TU Sikingine .! Si kingine But Juu ya Maisha Mengine Tulivyo Ishi Ama alinikera vipi Ama alinitesa Vipi sita weza kasema Kabisa, Coz alisha kuwa Mke Wangu na Sasa ni Mama wa watoto Wangu..Yeye kama ameweza Kuongea Uwongo Juu yangu na Juu ya Familia yangu akiwalazimishia Jamii ili mumuone yeye nimwanamke Shupavu sana alinivumilia But Mimi ndio Tatizo, Sawa Kabisa Mimi nimekubali kubeba Msalabua hu🙏 NISAMEHENI SANA Na sitarudia naOmba Kama u love my Music Please Support My Music sana Mwaka ndio Umeanza Nimeanza Na Mimi Kuwapa Burudani Nimeachia New video Inaitwa #Qualify link Iko kwa Bio Hapo Juu 👆👆 Support My Music Tuache haya Maisha yalio pita yapite coz haisaidii now Kila Mmoja Anamaisha yake ..Kujuwa Mimi ndio shida Ama Alio nizalia Watoto Ndio Shida Haisaidii Now ..NAWAPENDA SANA NAOMBA SUPPORT YENU TU YA MUSIC IF YOU LOVE MY MUSIC BASI ,#Hayamaishatu

View this post on Instagram

Guyz nawaomba Muwe Down Kabisa kwenye hili, Msinitukane wala Msimtukane Mzazi mwenzangu Coz Ukweli Haupo kamilifu ndani yenu katika kuamini hichi tunacho Zungumza .!! Bali kila Mmoja anahadisia tu Maisha yake yanyuma na Mwenza wake katika Alivyo mtenda kwa Ubaya Please nawaomba Mimi kama Mimi samahani 🙏 Coz Mimi sitaongelea Mapungufu ya Mwenza Wangu Kamwe, But kutokana na Maswali yenu juu ya Familia Yangu Yalikuwa Mengi,Na Mlishiliki katika Kutu Support juu ya Kuumwa kwake so Nikajaribu Kuongelea Kwa Nini Tulitengana Tu ..!! Na TATIZO NI CHITTING TU Sikingine .! Si kingine But Juu ya Maisha Mengine Tulivyo Ishi Ama alinikera vipi Ama alinitesa Vipi sita weza kasema Kabisa, Coz alisha kuwa Mke Wangu na Sasa ni Mama wa watoto Wangu..Yeye kama ameweza Kuongea Uwongo Juu yangu na Juu ya Familia yangu akiwalazimishia Jamii ili mumuone yeye nimwanamke Shupavu sana alinivumilia But Mimi ndio Tatizo, Sawa Kabisa Mimi nimekubali kubeba Msalabua hu🙏 NISAMEHENI SANA Na sitarudia naOmba Kama u love my Music Please Support My Music sana Mwaka ndio Umeanza Nimeanza Na Mimi Kuwapa Burudani Nimeachia New video Inaitwa #Qualify link Iko kwa Bio Hapo Juu 👆👆 Support My Music Tuache haya Maisha yalio pita yapite coz haisaidii now Kila Mmoja Anamaisha yake ..Kujuwa Mimi ndio shida Ama Alio nizalia Watoto Ndio Shida Haisaidii Now ..NAWAPENDA SANA NAOMBA SUPPORT YENU TU YA MUSIC IF YOU LOVE MY MUSIC BASI ,#Hayamaishatu

A post shared by Mabeste (@mabeste_tanzania) on

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW